Uingereza yasaini mkataba wa udhibiti wa Akili Mnemba
6 Septemba 2024Uingereza imeungana na Umoja wa Ulaya na Marekani katika kutia saini mkataba wa kwanza wa kimataifa kuhusu teknolojia ya akili mnemba. Mkataba huo unalenga kuyashinikiza mataifa kulinda watumiaji dhidi ya hatari zinazoweza kujitokeza kutokana na teknolojia hiyo. Mkataba huo ni wa kwanza wa kimataifa unaofungamana kisheria kuhusu teknolojia, ambao umekubaliwa na shirika la haki za binadamu la Baraza la Ulaya.Viongozi wa dunia wakutana Seoul kuijadili Akili ya Kubuni
Mkataba huo utazishinikiza nchi kufuatilia maendeleo ya teknolojia ya akili mnemba na kuhakikisha teknolojia hiyo inasimamiwa na sheria kali. Pia unajumuisha masharti ya kulinda taarifa za watumiaji. Wanaharakati wengi wametoa wito wa udhibiti zaidi na wa haraka wa teknolojia hiyo inayozidi kushamiri. Mwaka jana Uingereza iliandaa mkutano wa kwanza wa usalama wa teknolojia ya akili mnemba, uliohudhuriwa na viongozi wa ulimwengu na wakuu wa kampuni za teknolojia.