1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza kutanua ushirikiano wa ulinzi na Ujerumani

26 Septemba 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Lammy ameelezea nia ya taifa lake kutanua ushirikiano katika sekta ya ulinzi na Ujerumani pamoja na washirika wengine wa ulaya kutokana na tishio kutoka kwa Urusi.

https://p.dw.com/p/4l5FG
Ujerumani | Olaf Scholz akimkaribisha Keir Starmer
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer (kushoto) akiwa na Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Ebrahim Noroozi/AP Photo/picture alliance

Lammy amesema viongozi wa Magharibi wanatakiwa kuwa na wasiwasi kufuatia vita vinavyoendelea na kwamba wanapaswa kuimarisha ulinzi wao na uwezo wa kuzalisha silaha.

Kauli hiyo imetolewa wakati taarifa zinaeleza kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer atafanya ziara wiki ijayo mjini Brussels, Ubelgiji ambapo atakutana kwa mazungumzo na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen.

Soma pia: Keir Starmer apania kurudisha mahusiano mazuri kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya

Ziara ya Starmer inalenga kurekebisha mahusiano katika sekta ya biashara na usalama na washirika wake wa Ulaya baada ya miaka kadhaa ya mivutano, tangu Uingereza ilipojiondoa ndani ya Umoja huo.