Uingereza kuionya Israel kuhusu njaa katika ukanda wa Gaza
6 Machi 2024Kauli ya Cameron inatokea katika wakati ambapo ukosefu wa misaada unasababisha watu kufa kutokana na njaa katika ukanda wa Gaza.
Cameron ambaye anatarajiwa kukutana na mjumbe wa baraza la mawaziri la vita la Israel Benny Gantz hii leo, ameliambia bunge la Uingereza jana jioni kwamba jinsi Israeli inavyoshughulikia misaada ya wakaazi wa Gaza, inaibua maswali kuhusu uzingatiaji wake wa sheria za kimataifa.
Soma pia: Hamas yaahidi kuendelea na mazungumzo hadi makubaliano
Cameron ameliambia bunge hilo kwamba wiki kadhaa zilizopita alizungumzia kuhusu hatari ya kuzuka kwa baa la njaa na magonjwa na sasa hali imefikia kiwango hicho.
Waziri huyo ameongeza kuwa watu wanakufa kutokana na njaa na magonjwa yanayoweza kuzuilika.
Cameron ameliambia bunge hilo kwamba msaada uliopelekwa Gaza mwezi Februari ulikuwa karibu nusu ya kiwango kilichotolewa mwezi Januari.