Uhispania yapitisha sheria ya kubadilisha jinsia
16 Februari 2023Matangazo
Uhispania sasa inakuwa moja ya mataifa machache yanayoruhusu watu kubadilisha jinsia kwenye vitambulisho vya taifa kwa kufuata mchakato mwepesi wa kutangaza mabadiliko.
Bunge hilo pia limetoa idhini ya mwisho kwa sheria inayoruhusu likizo ya malipo ya matibabu kwa wanawake wanaopata maumivu makali wakati wa hedhi na kuwa taifa la kwanza barani Ulaya kuwa na sheria ya aina hiyo.
Soma pia:Dani Alves atuhumiwa kwa kumnyanyasa kingono mwanamke
Hatua hiyo lakini imeibua mgawanyiko miongoni mwa wanasiasa na vyama vya wafanyakazi, huku chama kikubwa cha wafanyakazi cha UGT kikionya inaweza kusababisha wanawake kunyanyapaliwa na wanaume wengi zaidi kuajiriwa.