Uganda yasaka ufadhili wa kuzalisha megawati 1,600 za umeme
2 Oktoba 2024Matangazo
Afisa wa Wizara ya Nishati nchini Uganda, Julius Namusaga, ametaja maeneo matatu muhimu yaliyoko kwenye Mto Nile, ambako mitambo hiyo inaweza kujengwa, na mkubwa zaidi ukiwa ni wa Ayago utakaozalisha megawati 840.
Soma zaidi: Pikipiki za bodaboda Uganda zatoa ajira na vurugu barabarani
Miradi mingine inayolengwa ni mtambo wa Kiba utakaozalisha megawati 400 na Oriang, megawati 392, na kufanya uzalishaji kufikia megawati 3,678 sawa na asilimia 80 ya uzalishaji wa sasa.
Hivi sasa, karibu asilimia 85 ya umeme wa Uganda unazalishwa na vituo vya umeme wa maji, na uliosalia unazalishwa na mitambo ya joto na jua.