Ufaransa yaongeza upekuzi mipakani kudhibiti uhamiaji
2 Oktoba 2024Matangazo
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Ufaransa Michel Barnier wakati alipozindua mpango mpya wa utawala wake bungeni jana Jumanne.
Barnier alisema udhibiti wa mpakani unaotarajiwa kufika mwisho mwezi huu wa Oktoba utarefushwa, akiangazia hatua kama hizo zilizochukuliwa nchini Ujerumani mwezi uliopita.
Soma zaidi: Ufaransa yaahidi kuimarisha uhusiano na Uingereza
Barnier pia aliahidi kuimarisha utendaji kwa ajili ya wakala wa ulinzi wa mipaka wa Ulaya, Frontex, ili kuboresha udhibiti na usimamizi wa mipaka ya nje ya Umoja wa Ulaya.