Ufaransa: Muungano siasa za shoto wamkosoa raia Macroo
11 Julai 2024Matangazo
Hakuna muungano ambao ulitoa mshindi wa moja kwa moja katika duru ya pili ya uchaguzi wa bunge, ingawa muungano mkubwa wa Wasoshalisti, Wakomunisti, Watetezi wa Mazingira, na chama cha LFI, chenye kufuata siasa kali za mrengo wa kushoto, ndiyo ulipata idadi kubwa ya viti kulivyo vyama vingine.
Muungano huo ulipata viti 193, katika bunge la taifa lenye viti 577.
Soma pia:Rais Macron atoa wito kwa vyama vikuu kushirikiana katika kuunda serikali thabiti ya Ufaransa
Katika barua ya wazi kwa wapiga kura, Macron alisema jana kuwa hakuna mtu aliyeshinda uchaguzi.
Macron amevitolea wito vyama kutafuta muafaka kwa ajili ya kuunda serikali ya mseto.