1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafaransa washiriki duru ya pili ya uchaguzi wa bunge

7 Julai 2024

Duru ya pili ya uchaguzi wa bunge inafanyika leo nchini Ufaransa, katika wakati ishara zinaonesha kwamba chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Rally (RN) huenda kitapata mafanikio katika uchaguzi huo.

https://p.dw.com/p/4hyly
Marine Le Pen
Kiongozi wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Rally (RN) nchini Ufaransa Marine Le PenPicha: Jerome Domine/abaca/picture alliance

Duru ya kwanza ya uchaguzi iliyofanyika tarehe 30 mwezi Juni ilitoa mafanikio makubwa kwa chama hicho kisichopenda wageni, kinachoongozwa na Marine Le Pen. Uchaguzi wa leo utaamua ni upande gani utakaodhibiti bunge na nani atakuwa Waziri mkuu wa Ufaransa.

Le Pen asema atapinga wanajeshi wa Ufaransa kupelekwa Ukraine

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, alichukua uamuzi ambao haukutarajiwa wa kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi mpya baada ya chama chake kushindwa vibaya katika uchaguzi wa bunge la Ulaya uliofanyika Juni 6 hadi 9. 

Iwapo hawatopata wingi wa kura bungeni, atalazimika kugawana madaraka na vyama vinavyopinga sera zake za biashara na kuwa karibu na Umoja wa Ulaya.