SiasaUfaransa
Ufaransa kujenga "ushirika sawa" na Afrika
6 Aprili 2024Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Stephane Sejourné amesema hayo siku ya Jumamosi.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari pamoja Sejourné amemwambia Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Musalia Mudavadi kwamba, wito wa Ufaransa utakuwa ni kujenga upya ushirikiano sawia na wenye kuheshimiana na nchi za Afrika na kwa manufaa ya mataifa yote.
Sejourné aliyeteuliwa mwezi Januari ameanza ziara yake ya kwanza barani Afrika le Jumamosi nchini Kenya na baadaye ataelekea Rwanda kabla ya kuhitimisha nchini Ivory Coast.
Uhusiano kati ya Ufaransa na mataifa kadhaa ya Afrika yaliyowahi kuwa makoloni yake, umedorora huku bara hilo likizidi kuwa uwanja wa vita vya kidiplomasia, hasa ushawishi wa Urusi na China ukiongezeka