1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ubelgiji yashutumiwa kwa kulipa fidia ya aibu, Iran

26 Mei 2023

Ubelgiji imeshutumiwa kwa kulipa fidia iliyotajwa kuwa "ya aibu" baada ya raia wake mmoja aliyetekwa nyara na Iran, kuachiliwa katika mabadilishano na mwanadiplomasia wa Iran aliyekutwa na hatia ya ugaidi nchini Ubelgiji

https://p.dw.com/p/4Rrwj
Belgien Terror-Prozess | Assadollah Assadi | Polizei
Picha: Dirk Waem/BELGA/Getty Images/AFP

Kundi la upinzani la Iran lenye makao yake mjini Paris, NCRI, limesema kwenye taarifa yake kwamba makubaliano kati ya mataifa hayo mawili yanaweza kuchochea kile lilichokiita "ufashisti wa kidini unaotawala Iran" na kuendeleza uhalifu wake kupitia ukandamizaji na ugaidi wa kikanda na kimataifa.

Mabadilishano ya wafungwa hao yaliyofanyika mapema leo, yalifikiwa licha ya miito ya kuipinga iliyotolewa na wanaharakati wa haki za binaadamu wa Ubelgiji na wanasheria.