Tunisia yakabiliwa na uhaba mkubwa wa sukari
2 Aprili 2024Matangazo
Kwa sasa, raia mmoja wa Tunisia hutakiwa kununua kilo moja hadi mbili ya sukari kwa wiki.
Nchini Tunisia, sukari hufadhiliwa na serikali kama ilivyo kwa bidhaa zengine muhimu za vyakula.
Lakini tangu mwishoni mwa mwaka 2022, nchi hiyo ya Afrika Kaskazini imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa fedha katika hazina ya umma na hivyo kusababisha uhaba wa bidhaa nyingine muhimu kama vile sukari na unga wa ngano.
Soma zaidi: Libya yafunga mpaka wake na Tunisia baada ya kuzuka mapigano
Katika miaka michache iliyopita, raia wapatao milioni 12 wa Tunisia wamekabiliwa na matatizo ya manunuzi kutokana na mfumuko wa bei, mdororo wa kiuchumi na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira. Inakadiriwa theluthi moja ya raia wa Tunisia wanaishi kwenye viwango vya umaskini.