Libya yafunga mpaka na Tunisia baada ya kuzuka mapigano
19 Machi 2024Wizara ya mambo ya ndani ya Libya imeamuru hii leo kufungwa "mara moja" kwa kituo kikubwa cha mpaka wake na Tunisia kufuatia mapigano yaliyozuka kati ya makundi yenye silaha na vikosi vya usalama vya upande wa Libya na kusababisha hali ya vurugu.
Kituo hicho kinapatikana katika jangwa la Ras Jedir takriban kilomita 170 kutoka mji mkuu wa Libya Tripoli, na ndicho kivuko kikuu kati ya nchi hizo mbili za Afrika Kaskazini. Hatua hii itawaathiri maelfu ya watu kusini mwa Tunisia ambao wanaishi kwa kutegemea biashara za mpakani. Libya yawarudisha makwao Wanigeria 161
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Libya, Imad Trabelsi, amesema hatua hiyo inalenga kuweka misingi ya kiusalama na kuhakikisha kazi za shirika la Posta zinafanyika chini ya mamlaka na uhalali wa serikali. Makundi hayo ya uhalifu yanatuhumiwa kuendesha shughuli za magendo.