1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Libya yawarudisha makwao Wanigeria 161

22 Agosti 2023

Mamlaka ya Libya imewarejesha makwao Wanigeria 161, kama sehemu ya mpango wa hiari wa wahamiaji kurudi makwao, mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa

https://p.dw.com/p/4VSWZ
Lybien Choucha Flüchtlinge Flash-Galerie
Picha: Gaia Anderson

Waandishi wa habari wa shirika la AFP wameeleza kuwa, watu hao, wakiwemo wanawake 75 na watoto sita, walipokea vyakula na vinywaji kutoka kwa wafanyikazi wa shirika la kimataifa la uhamiaji katika uwanja wa ndege wa Mitiga mjini Tripoli kabla ya kuabiri ndege.

Waziri wa mambo ya ndani wa Libya Imed Trabelsi, wa serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, alikutana na wahamiaji hao kabla ya wao kuondoka. Trabelsi amesema hawawezi kuwahudumia wahamiaji hao pekee yao bila ya msaada wa kimataifa huku akiongeza kati ya wahamiaji 161, watu 102 walinaswa kwenye mpaka walipokuwa wakijaribu kuvuka mipaka kati ya Libya na Tunisia.

Wahamiaji 15 wafa maji Libya

Mnamo Agosti 10, majirani wa Afrika Kaskazini , walikubaliana kugawana jukumu la kutoa makaazi kwa mamia ya wahamiaji waliokwama kwenye mipaka ya nchi hizo, na kumaliza mzozo wa mwezi mmoja uliosababishwa na kufukuzwa kwa wahamiaji na mamlaka ya Tunisia.