1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Tume ya uchaguzi yapigilia msumari ushindi wa Putin

21 Machi 2024

Tume ya uchaguzi nchini Urusi leo imetoa matokeo rasmi ya mwisho ya uchaguzi wa wiki iliyopita na kupuuzilia mbali ukosoaji mkali wa nchi za Magharibi na waangalizi huru kwamba uchaguzi huo ulikumbwa na kasoro nyingi

https://p.dw.com/p/4dz2V
Rais wa Urusi Vladimir Putin akizungumza wakati wa kampeini yake ya uchaguzi wa rais
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Gavriil Grigorov/POOL/TASS/dpa/picture alliance

Katika hotuba iliyotolewa kupitia vidio baada ya kuchapishwa kwa matokeo hayo yalioonesha kuwa Putin alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 87 ya kura, rais huyo aliwashukuru raia wa nchi hiyo kwa kumuunga mkono na kusema matokeo hayo yanaonesha uungaji mkono mkubwa wa sera zake.

Ikulu ya Kremlin yashtumu mataifa ya Magharibi

Ikulu ya Kremlin, leo imeyashtumu mataifa ya Magharibi kwa kuweka shinikizo lisilo la kawaida kwa benki za China zinazokubali malipo kutoka Urusi na kukiri kwamba kuna matatizo katika malipo ya kimataifa.

Soma pia:Urusi yafanya shambulizi la makombora mjini Kyiv

Maafisa wa Marekani na Ubelgiji wanazilenga kampuni na benki katika mataifa yanayoendelea ambayo zinasema zinaisaidia Urusi kuepuka vikwazo vya mataifa ya Magharibi kwa kufanya biashara na malipo.

Mamake Navalny ashindwa kesi

Mamake kiongozi wa upinzani wa Urusi aliyefariki dunia Alexei Navalny, ameshindwa katika kesi inayodai kuwa mwanawe hakupokea huduma nzuri ya matibabu akiwa gerezani. Haya yamesemwa na mshirika mmoja wa Navalny hii leo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwasili katika mkutano wa jumuiya ya kisiasa ya Ulaya mjini Granada nchini Uhispania mnamo Oktoba 5, 2023
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Thomas Coex/AFP

Ivan Zhdanov, msaidizi wa zamani wa Navalny, amesema mahakama hiyo iliyoko katika mji mdogo wa Labytnangi karibu na gereza la kikoloni alikofia Navalny, ilikataa kesi hiyo kwa misingi kwamba mlalamishi anapaswa kuwa Navalny mwenyewe.

Mkuu wa kamati ya kijeshi ya NATO afanya ziara nchini Ukraine

Mkuu wa kamati ya kijeshi ya jumuiya ya kujihami ya NATO Rob Bauer ameongoza ziara rasmi ya kwanza mjini Kyiv ya ujumbe wa kijeshi wa NATO tangu Februari 2022 wakati Urusi ilipotuma maelfu ya wanajeshi wake kuivamia Ukraine.

Bauer, ameuambia mkutano wa kiusalama wa Kyiv kwamba Ukraine inahitaji msaada zaidi na kwamba muda nchini Ukraine haupimwi kwa siku, wiki ama miezi lakini unapimwa kwa kigezo cha maisha ya watu.

Soma pia:NATO yajitenga na kauli ya Macron ya kuingiza jeshi Ukraine

Bauer pia ameipongeza Ukraine kwa ujasiri na uwezo wa kuingiliana na mazingira kwa haraka huku ikibadilisha masuala mengi ya vita vya kisasa.

Estonia yaahidi msaada zaidi kwa Ukraine

Waziri wa ulinzi wa Estonia Hanno Pevkur ameahidi msaada zaidi wa kijeshi kwa Ukraine wakati wa ziara mjini Kiev. Pevkur amemwambia mwenzake wa Ukraine Rustem Umerov kwamba Estonia italisaidia jeshi laUkrainekwa silaha na vifaa vya thamani ya dola milioni 21.8 katika vita vyake dhidi ya Urusi.

Pevkur ameongeza kuwa watatoa msaada huo kwa kuzingatia faidia kamili kwa Ukraine huku wakihakikisha kuwa hauathiri uwezo wa kuwa tayari kiulinzi wa nchi hiyo.