Tume ya haki Kenya yamtaka Mfalme Charles aombe msamaha
30 Oktoba 2023Matangazo
Mfalme Charles na mkewe Camilla hapo Jumanne watakuwa wanaanza ziara ya siku nne katika taifa hilo la Afrika Mashariki, hiyo ikiwa ziara yake ya kwanza kama mfalme katika nchi mwanachama wa Jumuiya ya Madola.
Kulingana na Kasri la Buckingham, Mfalme Charles anatarajiwa kuzungumzia "masuala yaliyoleta uchungu zaidi" katika uhusiani wa kihistoria kati ya Uingereza na Kenya.
Uingereza ilikubali kuwafidia zaidi ya Wakenya elfu 5 waliodhalilishwa na kuteswa wakati wa vita kupigania Uhuru vya Mau Mau, baada ya kesi iliyodumu kwa miaka kadhaa mahakamani.
Uingereza ilikubali kuwalipa fidia ya dola milioni 25.