Sheria na HakiMarekani
Trump kuhudhuria kesi dhidi yake katika Mahakama, Washington
9 Januari 2024Matangazo
Trump atatetea hoja yake mpya ya kwamba, kama rais wa zamani hapaswi kushtakiwa kwa tuhuma za kutaka kutengua matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.
Hukumu ya kesi hiyo inatarajiwa kutolewa Machi 4 mwaka huu mjini Washington katika chumba cha mahakama kilicho karibu na jengo la Bunge lililovamiwa na wafuasi wa Trump Januari 6 mwaka 2021.
Mawakili wa Trump wanajaribu kufuta mashtaka dhidi ya mteja wao kwa hoja mpya kwamba rais wa zamani ana "kinga kamili" na hawezi kufunguliwa mashtaka yeyote kutokana na hatua zake akiwa katika Ikulu ya White House.