Taliban yakosolewa kuwatenga wanawake katika mazungumzo UN
28 Juni 2024Utawala wa Taliban utakutana na wajumbe wa kimataifa siku ya Jumapili nchini Qatar katika kongamano la Umoja wa Mataifa la siku mbili kuhusu hali ya mambo Afghanistan, japo makundi ya kutetea haki za binadamu yameukosoa utawala huo kwa kuwatenga wanawake wa Afghanistan kwenye kongamano hilo.
Kongamano hilo la Umoja wa Mataifa linalojumuisha wajumbe 25 wakiwemo kutoka Marekani wanakutana mjini Doha mnamo Juni 30 na Julai mosi.
Soma pia:Vizuizi dhidi ya wanawake vyazidi kuitenga Afghanistan na jumuiya ya Kimataifa
Miongoni mwa ajenda ya mkutano huo ni pamoja na jinsi ya kupiga jeki uchumi wa nchi hiyo na kujadili ushirikiano wa kimataifa na Aghanistan hiyo ambayo inakabiliwa na migogoro chungunzima.
Tangu Taliban iliporejea madarakani mnamo mwaka 2021, utawala huo umepinga miito ya kuunda serikali inayojumuisha makundi yote ya kisiasa na kuhakikisha wanawake nchini humo wanapata haki ya elimu na pia kufanya kazi.