Taliban yahudhuria kikao kinachongozwa na Umoja Mataifa
30 Juni 2024Mkutano huo wa siku mbili ni watatu ili kujadili mzozo wa Afghanistan.
Soma pia: Taliban: Haki za wanawake wa Afghanistan ni suala la ndani
Kupitia mtandao wa kijamii wa X, msemaji mkuu wa serikali ya Taliban, Zabihullah Mujahid, ambaye anaongoza ujumbe huo amesema wamekutana na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Urusi, India na Uzbekistan.
Taliban hawakualikwa kwenye mkutano wa kwanza, ambao Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema masharti ya kuhudhuria kwao walitaka wanachama wa jumuiya ya kiraia wa Afghanistan kutengwa katika mazungumzo hayo na kwamba Taliban wachukuliwe kama watawala halali wa Afghanistan.
Hata hivyo, kufikia sasa hakuna nchi ambayo imeutambua rasmi utawala wa Taliban nchini Afghanistan, na Umoja wa Mataifa umesema itakuwa vigumu kutambuliwa kwa utawala huo, hasa kutokana na kuendeleza marufuku ya elimu na ajira kwa wanawake.