Watu milioni 55 wakabiliwa na njaa Afrika Magharibi na Kati
13 Aprili 2024Takriban watu milioni 55 wanakabiliwa na kitisho cha njaa katika kanda ya Afrika Magharibi na Kati kutokana na kupanda kwa bei za vyakula.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Shirika la Mpango wa Chakula duniani WFP, Shirika la kuhudumia watoto UNICEF na lile la Chakula na Kilimo, imesema kuwa idadi ya watu waliokabiliwa na njaa wakati wa msimu wa mavuno imeongezeka mara nne katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.Zimbabwe yatangaza ukame kuwa janga la kitaifa
Changamoto za kiuchumi ikiwa ni pamoja na mfumuko mkubwa wa bei na kudorora kwa uzalishaji wa ndani, vinatajwa kuchochea zaidi mgogoro huo wa njaa.
Mashirika hayo yameonya kuwa watoto wapatao milioni 17 walio chini ya umri wa miaka mitano wana utapiamlo kutokana na uhaba wa chakula.
Nchi zilizoathirika zaidi ni Nigeria, Ghana, Sierra Leone, na Mali.