Takriban raia 20 wauawa katika shambulizi nchini Kongo
26 Januari 2024Shambulizi hilo lilifanyika katika mji wa Mweso eneo la Masisi umbali wa takriban kilomita 80 kutoka mji wa Goma katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Maelezo ya pande husika yakinzana
Katika taarifa, jeshi limesema kuwa waasi hao wa M23 walirusha mabomu kuelekea Mweso wakati walipokuwa wakirudi nyuma kuepuka operesheni ya kijeshi dhidi yao.
Soma pia:Mapigano kati ya kundi la M23 na Wazalendo yazua hofu Kongo
Kwa upande wake, kiongozi wa M23 Bertrand Bisimwa, amelishtumu jeshi hilo kwa kutumia droni na silaha nzito kushambulia maeneo ya makazi katika mji huo wa Mweso.
Soma pia:M23 wakamata mji mashariki mwa Kongo
Katika taarifa aliyochapisha katika mtandao wa X, Bisimwa amesema mashambulizi hayo yamewauwa watoto, wanawake na wanaume na kuharibu nyumba, makanisa na shule.