Taiwan yasema China yafanya majaribio ya kivita
25 Septemba 2024Taarifa iliyotolewa siku ya Jumatano (Septemba 25) na wizara hiyo ilisema kuwa imezitambuwa ndege 23 za kivita zikifanya shughuli zake kuzunguka kisiwa hicho.
Taarifa hiyo inajiri wakati China yenyewe ikisema kuwa jeshi lake limefanikiwa kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu yanayoweza kuvuuka mabara kwenye Bahari ya Pasifiki.
Soma zaidi: China yaionya Ujerumani baada ya meli yake kupita Taiwan
Hata hivyo, taarifa ya wizara ya ulinzi ya China ilisema kwamba majaribio hayo hayakuelekezwa nchi wala shabaha yoyote na kwamba yalifanywa kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Harakati za kijeshi za China kwenye eneo hilo zimekuwa zikizusha wasiwasi kwamba huenda Beijing inakusudia kutumia nguvu za kijeshi kutwaa mamlaka kamili ya kisiwa cha Taiwan, ambacho inakitambuwa kuwa ni sehemu ya miliki yake.
Taiwan ilijitangazia uhuru na kujitenga na China Bara.