1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yaionya Ujerumani baada ya meli yake kupita Taiwan

14 Septemba 2024

China imesema kitendo cha meli za kivita za Ujerumani kupita katika eneo la ujia wa Taiwan ambalo linaigawa China na Taiwan kunahatarisha usalama katika eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4kcmL
Ujerumani na China
China yaionya Ujerumani baada ya meli yake ya kivita kupita katika ujia wa TaiwanPicha: Jia Qing/dpa/picture alliance

China imesema kitendo cha meli za kivita za Ujerumani kupita katika eneo la ujia wa Taiwan ambalo linaigawa China na Taiwan kunahatarisha usalama katika eneo hilo.

Kapteni wa jeshi la wanamaji wa China, Li Xi, amesema leo Jumamosi kuwa tabia ya Ujerumani kupita katika eneo hilo kunatoa ishara mbaya katika masuala ya kiusalama na kwamba wanajeshi wa China wapo kwenye operesheni ya tahadhari na wako tayari kuchukua hatua dhidi ya kitisho chochote.

Soma zaidi. China yahimiza kuimarishwa kwa juhudi za amani duniani

Jana Ijumaa, meli ya kivita ya Ujerumani ilivuka katika eneo hilo la Taiwan kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya miaka 20, licha ya pingamizi kutoka kwa serikali mjini Beijing.

Meli hiyo ya kivita ya Ujerumani ilipita katika njia hiyo inayoshindaniwa ikitoka Korea Kusini kuelekea Ufilipino.