1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

China yaongeza shughuli za kijeshi kwenye anga la Taiwan

Hawa Bihoga
4 Novemba 2024

Wizara ya Ulinzi ya Taiwan imeripoti kuona ndege 35 za kijeshi za China zikielekea kusini kwa mazoezi zaidi ya kijeshi katika bahari ya Pasifiki, ikiwa ni siku ya pili mfululizo.

https://p.dw.com/p/4mXsE
Ndege ya kivita ya Taiwan
Ndege ya kivita ya TaiwanPicha: Anadolu/picture alliance

China, ambayo inaiona Taiwan kama sehemu ya himaya yake, inafanya operesheni za mara kwa mara za kijeshi karibu na kisiwa hicho ili kuimarisha madai yake ya umiliki.

Katika ripoti ya Jumapili, Taiwan ilibaini ndege 37 za China, zikiwemo za mashambulizi chapa J-16 na H-6, ambapo ndege 35 zilienda kwenye mafunzo ya umbali mrefu. 

Soma pia:China yaripotiwa kufanya mazoezi ya doria karibu na Taiwan

Wizara ya Ulinzi ya China haikutoa tamko kuhusu operesheni hizi. Siku ya Jumamosi, China ilifanya doria ya pamoja ya utayari karibu na Taiwan, na mwezi uliopita, ilifanya mazoezi makubwa kama onyo dhidi ya vitendo vya kutaka kujitenga.

Rais wa Taiwan, Lai Ching-te, anasisitiza kuwa ni wananchi wa Taiwan tu wanaopaswa kuamua kuhusu mustakabali wao, lakini amepuuziliwa mbali na China.