1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yaripotiwa kufanya mazoezi ya doria karibu na Taiwan

Sylvia Mwehozi
27 Oktoba 2024

Wizara ya ulinzi ya Taiwan imesema hii leo kuwa ndege na meli za kivita za China, zimefanya doria nyingine ya mapambano karibu na kisiwa hicho.

https://p.dw.com/p/4mHT2
Ndege ya kivita ya China SU-30
Ndege ya kivita ya China SU-30Picha: Shao Jing/Xinhua/ZUMA/picture alliance

Wizara ya ulinzi ya Taiwan imesema hii leo kuwa ndege na meli za kivita za China, zimefanya doria nyingine ya mapambano karibu na kisiwa hicho. Hatua hiyo inajiri baada ya Beijing kutishia kuchukua hatua za kukabiliana na mpango wa Marekani wa mauzo ya dola bilioni 2 ya silaha kwa kisiwa hicho.Taiwan: Ndege 153 za kijeshi za China zashiriki mazoezi ya kijeshi Taiwan

Taarifa ya wizara ya ulinzi ya Taiwan imesema leo kuwa imegundua ndege za kivita zipatazo 19 za China, ikiwemo ndege ya Su-30, zikifanya mazoezi ya utayari karibu na kisiwa hicho. Mapema siku ya Ijumaa, wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon, iliidhinisha mpango wa mauzo ya silaha wa dola bilioni 2 kwa Taiwan, ikiwa ni pamoja na kuwasilishwa kwa mara ya kwanza kwenye kisiwa hicho mfumo wa hali ya juu wa makombora ya ulinzi wa anga uliojaribiwa nchini Ukraine.