Marekani yaidhinisha mauzo ya silaha kwa Taiwan
26 Oktoba 2024Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeidhinisha kitita cha mauzo ya silaha cha dola bilioni mbili kwa Taiwan. Ikiwa ni pamoja na mifumo ya hali ya juu ya makomboraya kutoka ardhini hadi angani pamoja na rada, hatua ambayo inaweza kuikasirisha China.
Kulingana na shirika linalohusika na mauzo hayo, biashara hiyo inajumuisha mifumo kadhaa ya kuzuia ndege, pamoja na mfumo wa NASAMS na makombora 123 yenye thamani ya jumla ya dola bilioni 1.2. Hata hivyo uuzaji huo unatakiwa kuidhinishwa na bunge la Marekani.
China imeonyesha mara kwa mara hasira yake dhidi ya uungaji mkono wa kimataifa kwa Taiwan na kuishutumu Washington kwa kuingilia masuala yake ya ndani. China inadumisha uwepo wa karibu kila siku wa ndege za kivita, ndege zisizo na rubani na meli za kivita kandokando mwa kisiwa hicho.