1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Taiwan yamrai Scholz kuionya China kutotumia mabavu

12 Aprili 2024

Taiwan inatumai Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani anayejitayarisha kwa ziara nchini China ataionya serikali ya Beijing dhidi ya kutumia nguvu za kijeshi kutimiza dhamira yake ya kukidhibiti kisiwa hicho kinachojitawala.

https://p.dw.com/p/4egqt
Taiwan
mwakilishi wa Taiwan nchini Ujerumani, Shieh Jhy-WeyPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Katika mahojiano na shirika la habari la Ujerumani, dpa, mwakilishi wa Taiwan nchini Ujerumani, Shieh Jhy-Wey, amesema Scholz tayari aliutoa ujumbe kama huo alipoitembelea China mwaka 2022 lakini tangu wakati huo vitisho dhidi ya Taiwan vimeongezeka. 

Afisa huyo amesema kutokana na hali hiyo haitakuwa vibaya kwa Kansela Scholz kurejea matamshi yake bila kificho atakapokutana na viongozi wa China wakati wa ziara yake ya siku tatu inayoanza kesho Jumamosi. 

Taiwan, China zinaweza kutatua tofauti zao, asema rais wa zamani baada ya kukutana na Xi

Anatarajiwa kufanya mazungumzo na Rais Xi Jinping na maafisa wengine wa ngazi ya juu wa utawala wa nchi hiyo ambayo kwa sehemu kubwa yatajikita kwenye masuala ya biashara.