Taiwan na China zinaweza kutatua tofauti zao kwa amani
11 Aprili 2024Ma ameongeza kuwa watu wa pande zote mbili za Mlango Bahari wa Taiwan wana utamaduni na historia inayofanana. Ma, alikuwa rais kuanzia 2008 hadi 2016, na mwaka jana alikuwa rais wa kwanza wa zamani wa Taiwan au aliyeko madarakani kuzuru China.
Ma Ying-jeou , alifanya mkutano wake wa pili na Xi, kufuatia mkutano wa kilele wa kihistoria nchini Singapore mwaka wa 2015 wakati Ma alikuwa bado kiongozi wa Taiwan. Ilikuwa ndio mara ya kwanza kwa viongozi wa Taiwan na China kukutana kufuatia kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika mwaka wa 1949.
China yalaani ziara ya ujumbe wa Marekani, Taiwan
China inaizingatia Taiwan inayotawaliwa kidemokrasia kuwa sehemu ya himaya yake, na imeongeza shinikizo la kijeshi na kisiasa ili kuyalazimisha madai hayo. Serikali zote mbili hazitambuani.