1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taiwan inamshikilia raia wa China kwa tuhuma za uvamizi

14 Oktoba 2024

Walinzi wa Pwani ya Kisiwa cha Taiwan wamesema wamemkamata raia wa China kwa tuhuma za uvamizi. Mwanamume huyo amekamatwa wakati China ikiendelea na luteka za kijeshi kukizunguka Kisiwa hicho.

https://p.dw.com/p/4llcJ
Taiwan
Taiwan imesema imemkamata rais wa China kwa tuhuma za kuingia ncini humo kinyume cha sheria.Picha: CHINA'S PEOPLE'S LIBERATION ARMY/AFP

Walinzi wa Pwani ya Kisiwa cha Taiwan wamesema wamemkamata raia wa China kwa tuhuma za uvamizi. Mwanamume huyo amekamatwa wakati China ikiendelea na luteka za kijeshi kukizunguka Kisiwa hicho. 

Kulingana na walinzi wa pwani wa Taiwan, mtu huyo amekamatwa leo Jumatatu akiwa kwenye mashua ndogo akijaribu kuvuka kuingia katika kisiwa kidogo cha Menghu kinyume cha sheria. 

Soma pia: China yafanya luteka za kijeshi karibu na Taiwan

Video iliyochapishwa na mamlaka za Taiwan iliwaonesha walinzi hao wakimfunga mikono mtuhumiwa huyona kwenda naye katika mashua yake ambako walipelekwa Kinmen kwa uchunguzi zaidi. 

Menghu ambako ni sehemu ya visiwa vya Kinmen chini ya Taiwan inayojitawala iko kilometa sita kutokamji wa bandari wa Xiamen mkoaji Fuijian eneo lililo China bara. China inaichukulia Taiwan inayojitawala kuwa ni sehemu yake.