1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yafanya luteka za kijeshi karibu na Taiwan

14 Oktoba 2024

China imeanzisha luteka za kijeshi katika maeneo yanayoizunguka Taiwan. Haya ni kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya China ambayo imetuma ndege na meli kuzingira kisiwa hicho kinachojitawala kidemokrasia.

https://p.dw.com/p/4ljz0
Kikosi maalum cha wanamaji wa Taiwan wakati wa mazoezi dhidi ya uvamizi wa China katika kisiwa cha Kinmen mnamo 29.08.2019
Kikosi maalum cha wanamaji wa Taiwan wakati wa mazoezi dhidi ya uvamizi wa China katika kisiwa cha KinmenPicha: Patrick Aventurier/abaca/picture alliance

China imesema kuwa luteka zake za kijeshi zilizopewa jina Joint Sword-2024A, zilikuwa na lengo la kupima uwezo wa pamoja wa vitengo vya kijeshi chini ya kamandi moja.

Msemaji wa kamandi ya mashariki ya China Li Xi, amesema mazoezi hayo yanafanyika katika maeneo ya kaskazini, kusini na mashariki mwa Taiwan.

Soma pia:Taiwan iko katika tahadhari kufuatia jaribio la kombora la China

Li ameongeza kuwa luteka hizo zinalenga doria za utayari wa vita pamoja na vizuizi kwenye bandari muhimu na maeneo.

Katika taarifa yake siku ya Alhamisi, kiongozi wa TaiwanLai Ching-te, aliapa kupinga unyakuzi wa kisiwa hicho na kusisitiza kuwa Beijing na Taipei haziko chini ya mamlaka au udhibiti wa mwingine.