1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSyria

Syria: Watoto wazidi kuajiriwa na makundi ya wapiganaji

5 Julai 2023

Idadi ya watoto wanaoandikishwa kwenye makundi ya wapiganaji nchini Syria inazidi kuongezeka licha ya mapigano ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kupungua.

https://p.dw.com/p/4TRMA
Syrien | al-Hol Camp in dem Familien von IS-Mitgliedern untergebracht sind
Picha: Baderkhan Ahmad/AP/picture alliance

Hivi karibuni binti mdogo wa miaka 13 akiwa ametoka kufanya mtihani shuleni  alipotea na baadaye kufahamika kwamba alikuwa amepelekwa katika moja ya makundi ya wapiganaji kaskazini mwa Syria.

Msichana huyo wa kikurdi alipotea njiani akiwa anarudi nyumbani kutoka shule ambako alienda kufanya mtihani wa shule mwezi uliopita , akiwa njiani alifikiwa na mtu anayetajwa kutokea katika kundi la wapiganaji,  wazazi wake wana hofu kubwa kwamba huenda binti yao alishawishiwa  kujiunga na kikundi chenye silaha na kwamba amepelekwa katika moja ya kambi kwa ajili ya mafunzo.Mashambulio Syria: Raia 10 wauawa miongoni mwao watoto wanne

Msichana, Peyal Aqil, alikuwa na marafiki zake walipokutana  na mwanaume ambaye baadae aligeuka kuwa kama mwajiri wa kundi lenye silaha linalotajwa kuwa ni Kundi la Vijana wa Mapinduzi. Anasema kuwa "Ilikuwa ni siku ya mtihani shuleni akatuacha mimi na baba yake , basi baada ya mtihani hakurudi tena".

Mwanaume huyo alimfuata binti huyo hadi kwenye kituo  cha mji uliopo kaskazini mwa Syria wa Qamishli ambapo marafiki zake walikuwa wakimsubiri nje lakini hakuweza kutokea tena.

Mama yake Peyal, Hamrin Alouji, anasema kwamba  yeye na mumewe wamelalamika kwa mamlaka za mitaa kwa muda bila mafanikio.

"Mimi na baba yake tumezunguka huku na kule, Nimemkumbuka sana na hapa ndio chumbani kwake, nakaaa tu ndani ingawa kila mmoja ananiambia nitoke nje kidogo, Nawaogopa hao watu wa kaskazini angekuwepo mwanangu ningempa hata juisi."

Kifusi mjini Idlib
Mtoto akicheza chini ya kifusi huko Idlib SyriaPicha: Juma Muhammad/ZUMA/picture alliance

Makundi yenye silaha nchini Syria yameajiri watoto katika kipindi cha miaka 12 iliyopita migogoro na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa kuhusu ajira ya hivi watoto ya karibuni inaeleza kwamba kuna ongezeko kubwa la matumizi ya askari watoto nchini Syria licha ya ukweli mapigano katika maeneo mengi ya Syria yanazidi kupungua.

 Idadi ya watoto waliosajiliwa na makundi yenye silaha nchini Syria imeongezeka kwa kasi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita kutoka 813 mwaka 2020 hadi 1,296 mwaka 2021 na 1,696 mnamo 2022.

Kulingana na ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa nusu ya kesi hizo zinahusisha makundi yenye silaha yalioko upande wa kaskazini mashariki mwa Syria.

Bassam Alahmad, Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kiraia inayoshughulikia masuala ya Ukweli na Haki nchini Syria amenukuliwa akisema kwamba watoto ni chungu nzima wanaolazimishwa kuingia katika makundi hayo ya kijeshi huku familia nyingine zikiwaruhusu watoto ili wapate pesa na kama ishara ya kuonesha uaminifu.

Juhudi za kukomesha uandikishaji kama huo zimekuwa ngumu na makundi yenye silaha yanayofanya kazi katika kila sehemu ya Syria.

Mwaka 2019,  Muungano wa wanamgambo wa kikabila na makundi ya waasi Kaskazini na Mashariki mwa Syria(SDF) ulitia saini ya makubaliano na Umoja wa Mataifa kuahidi kukomesha uandikishaji wa watoto chini ya miaka 18.

 Kundi hili mshirika wa Marekani ndio kundi pekee ambalo liliitikia wito wa Umoja wa Mataifa wa kukomesha matumizi ya askari watoto ingawa makundi mengine bado yanaendelea na utaratibu huo.

Syria Aleppo
Watoto katika kambi ya wakimbizi mjini Aleppo SyriaPicha: Juma Mohammad/Zuma/picture alliance

Wakati ripoti ya mwaka 2022 ya Umoja wa Mataifa ikihusisha kesi 10 za Vijana wa Mapinduzi, Asasi ya Kiraia inayoongozwa na Alahmad inaonesha kwamba  kundi la Vijana wa Mapinduzi liliwachukua watoto 45 kati ya 49 huku hizo zikiwa ni kesi zilizoripotiwa pekee.Mtoto mmoja kati ya wanne duniani wanaishi katika mazingira ya vita

Afisa mmoja wa kundi la Vijana wa Mapinduzi alikiri kuwa kikundi hicho linaajiri watoto lakini si kweli  kwamba wanawaandikisha kwa nguvu na wala hakuna anayelazimishwa na alipoulizwa kuhusu binti Peyal, alisema kwamba msichana huyo alijiunga na kundi hilo na alilalamika kutokuwa na furaha nyumbani kwao  na kwamba wazazi wake wamekuwa wakimlazimisha  kuvaa hijabu, Ingawa mama yake Alouji aliipiga kauli hiyo.

Mwezi mmoja baada ya kutoweka kwake Mei 21, Peyal amerudi nyumbani. Akikimbia katika moja ya kambi ya mafunzo ya kijeshi ya kikundi hicho, Hali ya binti huyo ikiwa na hali dhaifu na Alouji anasema familia kwa sasa ina hofu na kwamba usalama ni mdogo na wanafikiria kuondoka nchinin Syria.