1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Sudan yatuhumu Umoja wa Falme za kiarabu kuendeleza mzozo

Angela Mdungu
12 Septemba 2024

Serikali ya Sudan imeutupia lawama Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kuwapa silaha mahasimu wake wa kikosi cha jeshi kilichoasi, RSF, na imeonya kuwa hatua hiyo inauendeleza mzozo uliodumu kwa takriban miezi 7 nchini humo.

https://p.dw.com/p/4kXZp
Mzozo wa Sudan.
Jengo lililoshambuliwa na baada ya mashambulio ya pande zinazozozana Sudan.Picha: Mudathir Hameed/dpa/picture alliance

Upande wa jeshi la taifa unaoongoza nchi umetoa shutuma hizo katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo wanachama 15 wa umoja huo wamepiga kura ya kuongeza vikwazo vya silaha kwa mwaka mmoja katika imbo la Darfur ambalo ni eneo muhimu la mapambano kati ya jeshi na kikosi cha RSF kinachoongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Daglo. 

Soma pia:Shirika la HRW lasema pande hasimu Sudan zimenunua silaha kutoka nje

Kwa upande wake Umoja wa Falme za Kiarabu imezitaja tuhuma za Sudan kuwa ni za uongo na zisizo na msingi wowote. Nchi hiyo imeitupia lawama serikali ya Sudan kwa kushindwa kufanya mazungumzo ya usuluhishi na mahasimu wake ili kurejesha amani.