1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

HRW: Pande hasimu Sudan zimenunua silaha kutoka nje

10 Septemba 2024

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, limesema pande mbili hasimu za jeshi zinazopigana katika vita vya nchini Sudan zimenunua silaha na zana za kijeshi za kisasa kutoka nje.

https://p.dw.com/p/4kRVJ
Mapigano nchini Sudan
Mapigano nchini Sudan.Picha: Marwan Ali/AP/dpa/picture alliance

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya shiirika hiyo iliyochapishwa leo.

Shirika hilo limetoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kudurusu na kuupanua wigo wa vikwazo vya silaha vilivyowekwa dhidi ya jimbo la Darfur ujumuishe Sudan yote na pia imelitaka baraza hilo liwawajibishe wanaokiuka haki za binadamu.

Mtafiti mwandamizi wa migogoro wa asasi hiyo ya haki za binadamu Jean-Baptiste Gallopin, amesema mgogoro wa Sudan ni miongoni wa migogoro mikubwa duniani kutokana na pande husika kutenda uhalifu bila ya kuadhibiwa.

Amesema silaha mpya zilizopatikana huenda zikatumika kutenda uhalifu zaidi.