1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Sudan yataka mjumbe wa UN kuondolewa

27 Mei 2023

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ameshtushwa na barua kutoka kwa mkuu wa jeshi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan anayemuomba kumbadilisha mjumbe wake maalumu nchini humo Volker Perthes.

https://p.dw.com/p/4RtA0
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Volker Perthes, ambaye Jenerali Burhan anataka aondolewe.
Mzozo nchini Sudan unaibua wasiwasi kuanzia wa kiusalama hadi wa kijamii na kiutu baada ya wengi wa raia kuyakimbia makazi yao.Picha: ASHRAF SHAZLY/AFP/Getty Images

Hatua hii ya Jenerali Burhan inachukuliwa katikati ya mzozo unaoendelea nchini humo kati yake na aliyewahi kuwa msaidizi wake jenerali Mohammed Hamdani Dagalo.

Msemaji wa Guterres, Stephane Dujarric amesema kiongozi huyo ameshtushwa na ombi la kubadilishwa kwa mjumbe huyo, ambaye kulingana naye anafanya kazi nzuri kama mwakilishi wake.

Perthes na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo wamekuwa wakilengwa na waandamanaji wanaounga mkono jeshi ambao mara kwa mara wamekuwa wakimshutumu kwa uingiliaji wa kigeni na kutaka aondolewe.

Hii na hatua ya karibuni, katika msururu wa hatua zinazochukuliwa na mkuu huyo wa majeshi, ambaye wiki iliyopita alimfuta rasmi wadhifa wa umakamu, mpinzani wake Mohammed Hamdan Dagalo katika baraza tawala.

Soma Zaidi:Marekani, Saudia wasema usitishwaji mapigano Sudan unaheshimiwa kwa kiwango fulani