Ukraine itashinda vita iwapo itaendelea kupata msaada
30 Mei 2024Matangazo
Stoltenberg ametoa matamshi hayo muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi wanachama wa NATO nchini Jamhuri ya Czech.
Mkutano huo kwa sehemu kubwa utatawaliwa na suala la mzozo wa Ukraine hususani shinikizo linaloongezeka la kuyataka mataifa ya magharibi kutoa ruhusa kwa nchi hiyo kutumia silaha inazopokea kushambulia ndani ya Urusi.
Soma pia:Mawaziri wa kigeni wa NATO wanafanya mkutano Jamhuri ya Czech
Akizungumza mjini Prague, Stoltenberg amegusia suala hilo akisema ni wakati kwa washirika wa Ukraine kutafakari upya vizuizi vilivyopo kwa sababu vinahujumu uwezo wa nchi hiyo kujilinda dhidi ya Urusi.