MigogoroChina
Stoltenberg aitaka China iwajibishwe kwa kuiunga mkono Urusi
18 Juni 2024Matangazo
Stoltenberg ameeleza kuwa China inajaribu kutimiza malengo mawili kwa wakati mmoja, kwa kuiunga mkono Urusi kwa upande mmoja huku ikijaribu pia kudumisha uhusiano na mataifa ya Magharibi.
Ameishtumu China kwa kuuzidisha mzozo kati ya Urusi na Ukraine kupitia kile maafisa wa Marekani wanachosema kuwa Beijing inaisaidia Urusi kwa kuipa vifaa vya kijeshi.
Soma pia: NATO yajadili utayari wake wa silaha zake za nyuklia
China hata hivyo imetetea uhusiano wake na Moscow na kuzitaja ripoti za Marekani kama upotoshaji.
China imekwenda mbali zaidi na kusema, haitoi msaada wa silaha kwa pande yoyote katika mzozo kati ya Urusi na Ukraine, tofauti na inavyofanya Marekani na washirika wake wa Magharibi.