STOCKHOLM : Tuzo Mbadala ya Nobel kwa wanaharakati wa haki za binaadamu na mazingira
30 Septemba 2005Matangazo
Kile kinachojulikana kama Tuzo Mbadala ya Nobel itatolewa mwaka huu kwa wanaharakati wa haki za binaadamu na mazingira nchini Bhotswana,Canada,Malaysia na Mexico.
Hayo yametangazwa hapo jana na wakfu wa Tuzo ya Haki ya Kuishi ulioanzishwa na mfadhili Msweden na Mjerumani Jakob von Uexküll mjini Stockholm.
Tuzo hiyo yenye thamani ya zaidi ya euro 220,000 itatolewa mwezi wa Desemba katika bunge la Sweden.