1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Vifo vya bomu la kujitoa muhanga Somalia vyafikia 21

25 Septemba 2023

Idadi ya vifo vilivyotokana na bomu lililotegwa kwenye lori katikati mwa Somalia imeongezeka na kufikia 21 baada ya wafanyakazi wa huduma za dharura kuchimba vifusi na kupata miili zaidi iliyokuwa imefukiwa.

https://p.dw.com/p/4WkyJ
Wanamgabo wa Somalia wanashutumiwa kwa kusababisha ukosefu wa usalama nchini Somalia na mataifa jirani kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara.
Wanamgabo wa Somalia wanashutumiwa kwa kusababisha ukosefu wa usalama nchini Somalia na mataifa jirani kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara.Picha: picture alliance / AP Photo

Mtu aliyejitoa muhanga alilielekeza gari hilo lililokuwa limefurika vilipuzi kwenye kituo cha ukaguzi wa usalama katika mji wa Beledweyne jana Jumapili na kulipuka. Mlipuko huo uliharibu majengo yaliyo karibu na eneo hilo na kuwajeruhi baadhi ya wakazi.

Afisa wa polisi kwenye eneo hilo Ahmed Yare Adan amethibitisha idadi hiyo, iliyoongezeka kutoka 13 hadi 21 na kuongeza kuwa bado shughuli ya kutafuta miili inaendelea.

Kamanda msaidizi wa kituo cha polisi cha Beledweyne Sayid Ali kwa upande wake amesema mshambuliaji huyo alikilenga kituo cha basi chenye shughuli nyingi za biashara na majengo ya makazi.  

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amelaani shambulizi hilo na kuahidi kuimarisha vita dhidi ya kundi la Al-Shabaab wanaofanya uasi dhidi ya serikali kwa miaka 15 sasa.