1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Shirika la Msalaba Mwekundu laripoti vifo vya watu 22 Gaza

Sylvia Mwehozi
22 Juni 2024

Shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu limeripoti vifo vya watu 22 waliouwa katika shambulizi la makombora lililoharibu ofisi yake ya Gaza siku ya Ijumaa.

https://p.dw.com/p/4hNwt
Israel-Hamas | Shirika la Msalaba Mwekundu
Shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu GazaPicha: Ahmad Hasaballah/Getty Images

Shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu limeripoti vifo vya watu 22 waliouwa katika shambulizi la makombora lililoharibu ofisi yake ya Gaza siku ya Ijumaa. Ripoti hizo zinatolewa wakati jeshi la Israel likizidisha mashambulizi yake katika eneo la Palestina lililozingirwa.

Israel yashambulia katikati ya Gaza, yaingia ndani Rafah

Majibizano ya risasi katika mpaka wa Lebanon kati ya Israel na kundi la wanamgambo linaloungwa mkono na Iran la Hezbollah, yameongezeka katika wiki za hivi karibuni na kuibua wasiwasi wa kutanuka kwa vita.

Soma: Israel yatanua mashambulizi magharibi na kaskazini mwa Rafah

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema siku ya Ijumaa kwamba uhasama huo wa mpakani haupaswi kuigeuza Lebanon kuwa "Gaza nyingine" akionya juu ya kuzuka kwa janga jingine la kibinadamu.

Onyo lake limetolewa huku Israel ikizidisha mashambulizi katika Ukanda wa Gaza, ambako moja ya hospitali mjini humo imeripoti vifo vya watu 30.