Shambulizi la kigaidi laua wanajeshi 29 Niger
4 Oktoba 2023Matangazo
Waziri wa Ulinzi wa Niger, Luteni Jenerali Salifou Mody, amesema zaidi ya wapiganai 100 wanaotumia mabomu ya kuundwa nyumbani, wamekuwa wakiwalenga walinzi wa usalama wa taifa hilo ambao wapo katika ulinzi wa mpakani.
Hili ni shambulio la pili lenye kuwalenga wanajeshi wa Niger kwa juma hili pekee.
Hata hivyo Mody alionesha hali kudhibitiwa na nyenzo zao za vita kuteketezwa yakiwemo magari 15 na baadhi ya silaha kutekwa.
Utawala wa kijeshi ambao umechukua madaraka baada ya mapinduzi ya Julai dhidi ya serikali iliyochaguliwa kidemokrasia umetangaza siku tatu za maombolezo.