1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Serikali ya Ujerumani yalumbana juu ya bajeti

20 Juni 2024

Serikali ya Ujerumani ya vyama vitatu imeingia katika mzozo juu ya bajeti ya mwaka wa 2025 huku wataalamu wakitahadharisha kwamba huenda mzozo huo ukawa sababu ya kuvunjika kwa serikali hiyo.

https://p.dw.com/p/4hITO
Waziri wa Fedha wa Ujerumani Christian Lindner
Lindner anayetoka chama cha Waliberali, FDP anataka serikali ibanie kiasi cha Euro bilioni 30Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance/dpa

Waziri wa Fedha Christian Lindner anayetoka chama cha Waliberali, FDP anataka serikali ibanie kiasi cha takriban Euro bilioni 30. Vyama vingine vilivyomo katika serikali hiyo, vya Kijani na Social Demokratic, SPD vinapinga.

Wajumbe wa serikali hiyo ya pande tatu wanao muda wa hadi tarehe 3 Julai ili kufikia mwafaka. Serikali ya mseto ya Ujerumani imekuwa inakabiliwa na mivutano juu ya masuala kadhaa mnamo miezi ya hivi karibuni.

Wataalamu wanasema mzozo huo wa bajeti unaweza kuisambaratisha serikali ya mseto. Kulingana na taarifa ya wizara ya fedha, mapato ya kodi yanatarajiwa kupungua kwa Euro bilioni 11 mwaka ujao.