Lindner apinga kufufuliwa utumishi wa lazima jeshini
1 Aprili 2024Waziri Lindner ameliambia shirika la habari la dpa kuwa gharama za kiuchumi za mpango huo zitakuwa kubwa sana hasa katika wakati Ujerumani inakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi huku ikiwa na idadi kubwa ya watu wanaozeeka.
Ameongeza kuwa hajashawishika na pendekezo la kutaka watu wote wenye sifa kupatiwa mafunzo ya kijeshi bila uwezekano wa kuitwa kutumikia jeshini, na badala yake amependekeza kuundwa kikosi imara cha jeshi la akiba.
Soma pia: Berlin kusaka mwarobaini utekelezaji wa ukomo wa deni
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius hivi sasa anatathmini ruwaza za utumishi wa lazima jeshini, akichukuwa mifano kutoka mataifa ya Skandnavia.
Mafunzo ya lazima jeshini yalisitishwa nchini Ujerumani Julai 2011 baada ya miaka 55, lakini bado imeainishwa katika sheria kwamba utumishi wa lazima kwa wanaume utafufuliwa ikiwa kutatokea machafuko na kwa ajili ya ulinzi wa taifa.