1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Ufaransa yakabiliwa na kura mbili za kutokuwa na imani nayo

20 Machi 2023

Serikali ya Ufaransa inakabiliwa na kura mbili za kutokuwa na imani nayo baada ya wiki iliyopita Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Elisabeth Borne kulazimisha mageuzi yenye utata kuhusu pensheni, bila ya kupiga kura na bunge.

https://p.dw.com/p/4OvhN
Frankreich l Protest gegen die geplante Rentenreform in Lille
Picha: Sameer Al-Doumy/AFP

Mageuzi hayo yaliyoanzishwa na Rais Emmanuel Macronyataongeza muda wa kustaafu kutoka umri wa miaka 62 hadi 64.

Hatua hiyo imesababisha maandamano mjini Paris na kwenye miji mingine tangu Alhamisi iliyopita.

Mojawapo ya hoja ya kutokuwa na imani na serikali ya Rais Macron ilipendekezwa na chama cha Liot na kuungwa mkono na muungano wa siasa za mrengo wa kushoto wa Nupes.

Kura nyingine iliwasilishwa na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, National Rally cha Marine Le Pen. Iwapo kura hiyo itafanikiwa, muswada wa mageuzi ya pensheni utakataliwa na Macron atalazimika kuteua baraza jipya la mawaziri.