1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron akabiliwa na upinzani zaidi nchini mwake

17 Machi 2023

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anakabiliwa na shinikizo la maandamano na tuhuma za kuchukua uamuzi unaotajwa kuwa usio wa kidemokrasia baada ya kuidhinisha mageuzi tata ya pensheni bila ya kura ya bunge.

https://p.dw.com/p/4OpeH
Marseille Proteste nach Parlamentssitzung zu Rentenreform
Picha: CHRISTOPHE SIMON/AFP

Kwa kutumia mamlaka maalum ya kikatiba kupitisha sheria bila kura ya bunge, iliashiria kukiri kuwa serikali haina wingi wa kura katika uamuzi wa kuongeza umri wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 64, mabadiliko ambayo yamekumbwa na upinzani mkali kote nchini humo. Baraza la Seneti liliidhinisha mswada huo mapema jana, lakini kusitasita kwa wabunge wa upinzani wenye siasa za mrengo wa kulia kumuunga mkono Macron, kulimaanisha kuwa serikali ingeshindwa kuupitisha mswada huo bungeni. Usafiri wa treni, masomo shuleni, huduma za umma na bandarini tangu Januari zimeathirika na migomo ya kupinga mageuzi hayo, wakati kukiwa na maandamano makubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa katika miongo mingi.