Serikali ya Brazil yadhibiti umiliki wa bunduki
22 Julai 2023Hatua hii ni kutaka kutengua sheria zilizochochea ongezeko la umiliki wa bunduki zilizoungwa mkono na mtangulizi wake Jair Bolsonaro.
Da Silva amechukua hatua hiyo ikiwa ni msururu wa hatua za kukabiliana na ghasia mjini Brasilia, baada ya kuripotiwa kwa visa kadhaa vya ufyetuaji risasi mashuleni. Amri ya rais huyo wa Brazil itawafanya watu kumiliki silaha mbili pekee kwa matumizi ya ulinzi binafsi.
Soma pia: Bolsonaro ahojiwa kwa njama za kumzuwia Lula madarakani
Chini ya amri hiyo, mtu yeyote anayetaka kupata bunduki atalazimika kuthibitisha kuwa anaihitaji. Wawindaji na wanaotumia bunduki katika michezo watapunguziwa idadi ya silaha hadi sita, kutoka 30 walizokuwa wakiruhusiwa kumiliki hapo awali.
Wakati wa utawala wa Bolsonaroumiliki wa bunduki kwa matumizi binafsi uliongozeka maradufu baada ya kulegeza masharti ya umiliki wa silaha.