Serbia, Kosovo wakutana kwenye mazungumzo ya kusakaa suluhu
14 Septemba 2023Rais wa Serbia Aleksandar Vucic na waziri mkuu wa Kosovo Albin Kurti wako Brussels kwa mazungumzo chini ya kile kinachoitwa mchakato wa mazungumzo wa Belgrade-Pristina, unaosimamiwa na mkuu wa sera za kigeni wa Ulaya, Josep Borrell.
Mikutano hii inafanyika hukumiito ikiongezeka ya mabadiliko katika mchakato wa kidiplomasia wa magharibi katika kuushughulikia mvutanouliopo, huku kukiwa na mashaka huenda ukasambaa na kushindwa kudhibitiwa.
Soma pia:Serbia yawaachia maafisa wa polisi wa Kosovo
Awamu ya mwisho ya mazungumzo mwezi Juni ilimalizika bila ya makubaliano yoyote.
Vucic na Kurti walikataa kukutana ana kwa ana na Borrell aliyekutana nao kwa nyakati tofauti alikiri kwamba wakuu hao walikuwa na "tafsiri tofauti za sababu, ukweli, matokeo na suluhisho la mvutano huo uliodumu kwa miongo kadhaa.