Seneta Vance: Trump hatoitelekeza NATO dhidi ya adui
18 Februari 2024Mtetezi mkubwa wa aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump katika bunge la Marekani, ametoa hakikisho kwa washirika wa NATO kuwa Marekani itashiriki katika utetezi wa mataifa wanachama pale itakapotokea uvamizi hata kama rais huyo atarejea kwa awamu ya pili katika kiti cha urais mwezi Novemba. Akizungumza na waandishi wa habari kandoni mwa mkutano wa usalama wa huko Munich Ujerumani, Seneta JD Vance, amesema, ujumbe kutoka kwa Trump na wanachama wenzake wa Republican ni kuwa, Ulaya inafaa iongeze nguvu binafsi, zaidi pale linapokuja suala la kujilinda. Vanceameongeza kusema iwapo Ulaya inaamini rais wa Urusi Vladimir Putin ni "tishio" basi mataifa yenye nguvu ya kiuchumi kama Ujerumani lazima yaingilie kati. Mkutano wa usalama unaofanyika Munich unahitimishwa hii leo, ambapo Marekani imetowa wawakilishi wake wakiwemo zaidi ya wajumbe 30 wa bunge la Marekani katika mkutano huo.