1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Scholz: Kitisho cha Urusi kutumia zana za nyuklia kimepungua

8 Desemba 2022

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema kitisho cha kutumia zana hatari za nyuklia katika mzozo wa Ukraine kimepungua kufuatia shinikizo la kimataifa dhidi ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4KgOQ
Olaf Scholz
Picha: Markus Schreiber/AP/picture alliance

Akihojiwa leo na shirika la habari la Ujerumani Funkte, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema jambo moja limebadilika, nalo ni kwamba Urusi imeacha kutishia kutumia silaha za nyuklia.

Alipoulizwa ikiwa kitisho cha nyuklia hakipo tena, Scholz alijibu kwa kusema kwa sasa tumetia kikomo dhidi ya kitisho hicho.Ukraine yapambana kurudisha umeme baada ya mashambulizi

Kiongozi huyo wa Ujerumani amepongeza ziara yake kuelekea China akisema imechangia hali hiyo ya sasa.

"Wakati wa ziara yangu Beijing, rais wa China Xi Jinping na mimi, kwa pamoja tulieleza kwamba silaha za nyuklia lazima zisitumike. Baada ya hiyo, nchi tajiri na zinazoinukia kiviwanda katika kundi la G20 zikasisitiza msimamo huo," amesema Scholz. 

Rais Xi, Kansela Scholz watafuta kuimarisha ushirikiano

Olaf Scholz asema kitisho cha Urusi kutumia silaha za nyuklia kimepungua kufuatia shinikizo dhidi yake kimataifa.
Olaf Scholz asema kitisho cha Urusi kutumia silaha za nyuklia kimepungua kufuatia shinikizo dhidi yake kimataifa.Picha: KCNA/KNS/STR/AFP

Matamshi ya Putin na mkwamo wa kijeshi, kwa pamoja zimezidisha hofu kwamba Urusi inaweza kutumia silaha za nyuklia kupata ushindi wa kijeshi katika mzozo wake na Ukraine.

Putin: Urusi kutumia silaha za nyuklia kama itashambuliwa nazo

Lakini alipozungumza na tume yake kuhusu haki za binadamu siku ya Jumatano, alisema nchi yake itatumia tu silaha za nyuklia kama jibu ikiwa kutakuwa na shambulizi la aina hiyo dhidi yao.

Hayo yakijiri rais wa urusi Vladimir Putin amesema Urusi itaendelea kushambulia miundombinu ya nishati ya Ukraine.Macron ataka Magharibi izungumze na Putin

 Amesema hayo mnamo wakati wizara ya Mambo ya Nje ya nchi yake pia ilitangulia kusema kuwa lengo kuu la eneo salama linalopendekezwa karibu na mtambo wa nishati ya nyuklia ya Zaporizhzhia kusini mwa Ukraine, ni kuzuia Ukraine kuushambulia mtambo huo.

Urusi na Ukraine zimekuwa zikinyosheana vidole vya lawama kufuatia mashambulizi yanayofanyika karibu na kinu cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzhia.
Urusi na Ukraine zimekuwa zikinyosheana vidole vya lawama kufuatia mashambulizi yanayofanyika karibu na kinu cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzhia.Picha: AP/picture alliance

Hofu ya janga la kinyuklia kufuatia mashambulizi Zaporizhzhia

Urusi na Ukraine zimekuwa zikitupiana lawama kuhusu mashambulizi karibu na kinu hicho kikubwa zaidi barani Ulaya. Kuna hofu kuwa mashambulizi katika mtambo huo, yanaweza kusababisha janga kubwa la kinyuklia.

Katika tukio jingine, Urusi imesema rasi ya Crimea ambayo iliimega mwaka 2014 ipo katika hatari ya mashambulizi kutoka Ukraine, baada ya maafisa katika rasi hiyo kusema walidungua ndege moja aina ya drone karibu na kambi yao moja muhimu ya jeshi la majini.

Msemaji wa serikali ya Urusi Dmitry Peskov amewaambia waandishi wa habari kwamba kuna vitisho kwa sababu Ukraine inaendelea na kile alichokitaja kuwa sera ya kupanga mashambulizi ya kigaidi.

(AFPE, RTRE)

Tafsiri: John Juma

Mhariri: Zainab Aziz