Scholz ataka waathirika wa Magdeburg wapatiwe msaada zaidi
7 Januari 2025Scholz ameliambia jarida la Stern kwamba anataka waathirika hao wawe na madai bora zaidi ya msaada wa serikali katika kushughulikia matokeo ya mkasa huo.
Kwa sasa, waathirika wa mashambulizi kama hayo wanaweza tu kupatiwa msaada ikiwa tukio limetambuliwa kuwa la kigaidi.
Soma zaidi: Idadi ya waliojeruhiwa katika shambulizi Ujerumani yaongezeka
Katika tukio hilo la tarehe 20 Disemba, mtuhumiwa mwenye uraia wa Saudi Arabia ambaye amekuwa akiishi hapa Ujerumani kwa miaka mingi, aliendesha gari lake kwenye umati uliokuwa wamejumuika katika soko la Krismasi na kuwauwa watu sita na kuwajeruhi wengine 299.
Kwa mujibu wa ofisi ya mwendesha mashitaka ya Naumburg, bado wanasaka ushauri wa kitaalamu kuamua endapo mtuhumiwa huyo, aliyetambuliwa kuwa mtu aliyeritadi na mwenye chuki dhidi ya Waislamu, ni mgonjwa wa akili.