Idadi ya majeruhi katika shambulizi Ujerumani yaongezeka
3 Januari 2025Matangazo
Taarifa hizo zimetolewa leo na wizara ya mambo ya ndani ya jimbo la Saxony-Anhalt. Idadi hiyo mpya inajumuisha watu waliojeruhiwa, ambao awali hawakusajiliwa, au waliripotiwa tu kwa mamlaka baada ya shambulizi hilo.
Kumi na mbili kati ya waliojeruhiwa ni raia wa kigeni au wana uraia wa nchi mbili. Desemba 20, mwanaume mwenye umri wa miaka 50, aliendesha gari na kuuparamia kwa makusudi umati wa watu soko la Krismasi katikati mwa mji huo na kusababisha vifo vya watu watano.