1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHungary

Scholz apuuza kuhusisha bajeti ya EU na fedha za Hungary

16 Desemba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema kuwa ameondoa uwezekano wa kuhusisha mazungumzo ya bajeti ya Umoja wa Ulaya, yanayojumuisha pia msaada kwa Ukraine, na kutolewa kwa fedha zilizozuiwa kwa Hungary

https://p.dw.com/p/4aF1G
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels mnamo Desemba 14, 2023
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: European Union

Baada ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels, Scholz amesema kuwa haipaswi kuchanganya masuala mawili yasiokuwa na uhusiano.

Soma pia:Umoja wa Ulaya washindwa kupata makubaliano kuisidia Ukraine

Kansela huyo wa Ujerumani alikuwa akijibu taarifa ya waziri mkuu wa Hungary, Viktor Orbán wakati wa mahojiano na shirika la habari la serikali ya Hungary iliyosema kuwa kwa Umoja wa Ulaya kutaka kubadilisha sheria ya miaka saba ya bajeti yake, ni fursa nzuri kwa Hungary kupata fedha nyingine zilizozuiwa.